habari Mpya


DC Ngara-Majeruhi 11 wa Bomu bado wako chini ya Uangalizi wa Madaktari Bingwa.

azam12
Madaktari wakiendelea kutoa huduma kwa majeruhi wa bomu ,hospitali ya Rulenge,Ngara.

Serikali ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, imesema Majeruhi 11 wa bomu waliolazwa katika Hospitali ya Misheni Rulenge wilayani humo wataendelea kuwa chini ya uangalizi wa Madaktari Bingwa waliotoka Hospitali ya Rufaa mkoa wa Kagera na Bugando.
IMG_20171109_104045

IMG-20171109-WA0016
Toka kushoto ni DC Ngara ,Luteni Kanali Mtenjele na Mkurugenzi wilaya ,Bw.Aidan Bahama wakiwa nyumbani kwa mmoja wa Wazazi wa Mtoto aliyejeruhiwa Kihinga.
 
Mkuu wa wilaya ya Ngara, Luteni Michael Mtenjele amebainisha hayo leo November 11, 2017, wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kwamba hali za Majeruhi hao zinaleta  matumaini kiafya kutokana na juhudi zinazofanywa na wataalamu wa afya.
 
Aidha amesema kwamba wagonjwa hao wanaendelea kuhudumiwa na waganga kwa kutibiwa majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji na hofu kubwa ilikuwa ni upungufu wa damu lakini wananchi wengi wamejitokeza kutoa damu salama kwa majeruhi hao.
IMG_20171109_134658
DMO wa Ngara Dr.revocatus Pichani Katikati na Watalamu wengine wa Afya kituo cha Rulenge wakiwa na Msaada wa Vifaa tiba.
 
 Luteni Kanali Mtenjele amesema kuwa tumepata msaada mwingine kutoka benki ya damu ya wilaya jirani ya Karagwe vikiwemo vifa tiba na dawa kutoka zahanati za jirani, MSD tawi la Muleba na Ofisi ya mganga mkuu wa mkoa.
 
Novemba 8,2017 katika Shule ya msingi Kihinga iliyopo kata ya Kibogora ,wilayani Ngara ulitokea mlipuko wa bomu uliosababisha vifo vya Wanafunzi Watano wa Darasa la kwanza pamoja na Majeruhi baada ya Mwanafunzi mmoja kufika na bomu hilo shuleni hapo akidhani kwamba ni chuma chakavu.

Post a Comment

0 Comments