habari Mpya


Arsenal yaigonga 2-0 Tottenham,yabaki Nafasi ya 6.

2
Arsenal imeitandika magoli 2 – 0 kwenye muda wa  kipindi cha kwanza na kuwalaza wapinzani wao wa jadi mjini London, Tottenham kwa mara ya kwanza katika mechi saba za ligi ya Uingereza jioni ya Leo November 18, 2017.

Beki Shkrodan Mustafi alifunga kwa kichwa kizuri kutoka kwa krosi iliopigwa na Mesut Ozil , lakini Spurs wanadai kwamba mpira wa adhabu uliopigwa baada ya Davinson kumchezea visivyo Alexis Sanchez ulikuwa uamuzi mkali.
1

3
The Gunners waliongeza bao la pili dakika tano baadaye , baada ya mshambuliaji wa Chile, Sanchez kufunga krosi iliopigwa na Alexandre Lacazzette akiwa amekaribia goli.
 
Sanchez alikuwa na fursa ya kuongeza bao la tatu lakini shambulio lake likapanguliwa na Hugo Lloris.
 
Fursa nzuri ya wageni hao ilimwangukia kiungo wa kati Christian Eriksen katika kipindi cha kwanza lakini shambulio la kimo cha paka la raia huyo wa Denmark liligonga chuma cha goli huku kipa Petr Cech akiruka na kuokoa kichwa kilichopigwa na Eric Dier.
4

5
Ushindi huo sasa umeifanya Arsenal kubaki nafasi ya 6 katika Msimamo wa Ligi msimu huu 2017/2018 wakiwa na Pointi 22  juu ya kikosi cha Mauricio Pochettino chenye Pointi 23 nafasi ya 4.
6

Post a Comment

0 Comments