habari Mpya


Rais Magufuli Apinga Nyongeza ya Posho kwa Madiwani,Awataka Wakurugenzi Kutatua Migogoro katika Maeneo yao Haraka.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka Madiwani wasio na Shughuli ya kuwaingizia Pesa binafsi kujiuzulu, kwani Serikali yake haiwezi kuwaongezea posho wanayohitaji.
 
Akizungumza kwenye uzinduzi wa mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es salaam, amesema kwamba Madiwani hao walifahamu masharti ya kugombea nafasi hiyo, hivyo kama wameshindwa kuyatimiza ni vyema wakajiuzulu.
 
Ndio maana diwani masharti tunapojaza fomu tunaambiwa lazima uwe na kazi maalum inayokupa kipato, sasa kama wapo madiwani waliojaza hiyo nafasi na hawana kazi ya kuwapa kipato, wajiuzulu udiwani”, amesema Rais Magufuli.
 
Leo katika hotuba iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli ikisomwa na Mwenyekiti wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) Bwana Gulam Mkadam, waliomba kuongezewa posho za madiwani, kutoka Tsh. 300,000 hadi Tsh. 800,000 jambo ambalo Rais amelipinga. 
 
Katika hatua nyingine,Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kuwafukuza kazi Wakurugenzi wa halmashauri wanne kwa ulevi wa pombe pindi wawapo makazini.
 
"Nimepata taarifa ya Wakurugenzi kama wawili watatu hivi ni walevi sana, nawaambia hao wataondoka kama upo hapa Mkurugenzi halafu ni mlevi ukajirekebishe haraka sana, kabla sijaja huko ili angalau uonekane umebadilika" alisema Rais Magufuli. 
 
Mbali na hilo Rais Magufuli aliwataka viongozi hao kwenda kumaliza migogoro mbalimbali ndani ya halmashauri zao na mivutano isiyokuwa na msingi na kusema kuwa vyama vya siasa si adui bali adui wa kwanza wa serikali yake ni watu wanaokuja kuiba maliasili za Tanzania. 
 
"Haipendezi kuwa na makundi, muyamalize makundu hayo kwenye manispaa, tunajenga nyumba moja adui yetu siyo vyama tunachelewa sana, adui yetu ni wale wanaotuibia nasema mkamalize hayo makundi huko, najua tofauti lazima zitakuwepo lakini kwenye masuala ya kazi lazima tushikamane kwa maslahi ya Watanzania, mkawaimize Watanzania kufanya mambo ya maendeleo" alisisitiza Rais Magufuli

Post a Comment

0 Comments