habari Mpya


Mahafali ya 35 Kidato cha Nne Rulenge Sekondari ( Mt Alfred Rulenge ) 2017 Yavutia.

Picha Juu na Chini; Wahitimu wa Kidato cha Nne Rulenge Sekondar wakionesha maigizo wakati wa Mahafali ya 35 yaliyofanyika Shuleni hapo Leo October 13,2017.

Habari/Picha: Shaaban Ndyamukama.

Mkuu wa shule ya sekondari ya Mtakatifu Alferd Rulenge  inayomilikiwa na jimbo katoliki la Rulenge Ngara mkoani Kagera Padre Emanyel Nzeymana  amesema wahitmu wa kidato cha nne shuleni hapo mwaka huu Walianza mwaka 2014 wakiwa 154 kati yao Wavulana 72  huku Wasichana wakiwa 82 ambapo hadi leo  Wamehitimu 133, Wasichan 64  na Wavulana 69 na baadhi hawakumaliza kwa sababu za  kuhama kwa utovu wa nidhamu.

Shule hiyo inafanya vizuri kitaaluma na kufaulu mitihani ya aina mbalimbali kuanzia ngazi ya shule hadi kitaifa.

Mikakati iliyopo nikuongeza muda wa kujisomea na wanafunzi kujengewa misingi ya kinidhamu.
Wahitimu pichani, waliweza kushiriki katika kuanzisha miradi ya ujasiliamali , michezo, na kushiriki malezi ya kiroho bila kujali tofauti za madhehebu yao na hii ni mipango ya ufanisi wa shule hiyo.

Shule inayo miradi ya kilimo na ufugaji kwa kuwapatia elimu ya kujitegemea na mafunzo ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ili wanapohitimu elimu ya sekondari waweze kujikwamua kiuchumi.Mojawapo ya miradi yenye kufurahisha walimu na wanafunzi kwa wiki mbili zilizopita wakiwemo wafanyakazi ni kupatikana kuchimbwa kwa kisima cha maji ambayo ni moja ya changamoto ya muda mrefu ambapo kero ya pili ilikuwa ni umeme ambao umefungwa na REA utakaoingia hadi chanzo cha maji ya mto Mpanyura

Changamoto.

Upungufu wa vyumba vya madarasa na baadhi ya majengo kuchakaa baada yakuongezeka kitengo cha taasusi ya sayansi na visima vya kuvuna maji ya mvua hivyo waliowahi kusomea katika shule hiyo kutumia elimu na mapato yao kusaidia kuboresha miundombinu iliyokuwa ikitumika kuwainua kitaaluma.

Wosia kwa Wahitimu.

Kuhakikisha wanatumia elimu na malezi kudumisha nidhamu na maadili mema kwenye jamii watakapokuwa wakitoa huduma mbalimbali kupitia vipaji na fani watakazoendelea kupata ndani na nne ya nchi.

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliohitimu na wanaoendelea na masomo wameupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuwapatia kisima cha maji kuwaondolea kero ya maji ya muda mrefu  kwa kuvunja ratiba ya kufuata maji mto Mpanyula na sasa wanaomba gari la kusafria

Mgeni rasmi,  Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera, Alex Gashaza aliyewakilishwa na  Afisa Elimu Idara ya Msingi kitengo cha Elimu ya watu wazima  Bw Frank  Kitunzi  ambaye amesema Wahitimu hawana budi kufanya shughuli za kusaidia wazazi na jamii inayowazunguka ikiwa  ni pamoja na kutunza mazingira pia kushiriki matukio ya kijamii  kuleta hamasa ya kuwaendeleza kitaaluma.

Pia amesema kujihadhari na maadili mabaya kwa kutumia madawa ya kulevya ya aina mbalimbali na kujihadhari kuendesha vyombo vya moto bila kuzingatia sheria za usalama barabarani na katika maisha yao kufunga nadhiri na pingu za ndoa takatifu kwa kuepuka anasa zinazomchukiza mungu.

Kwa upande wa wazazi kuendelea kutoa malezi ya kiroho , kwa mila na desturi kufuata tamaduni halali za kitanzania na afrika kuelekea uchumi wa kati na wa viwanda

Katika mahafali hayo Mbunge  Alex Gashaza ameahidi Shilingi laki tano kuweza kupunguza changamoto za shule hiyo hasa kununua vifaa vya ujenzi wa chumba cha darasa kwa ajili ya kufundishia masomo ya sayansi kwa vitendo.


Post a Comment

0 Comments