habari Mpya


VPL Tanzania Bara -Yanga SC waifumua Njombe Mji nyumbani.

Mabingwa watetezi wa VPL Tanzania bara ,Yanga SC  Jana September 10,2017 wamevuna pointi tatu za kwanza katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Njombe Mji Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.

Shukurani kwake, mshambuliaji mpya, Ibrahim Hajib Migomba aliyefunga bao hilo pekee kipindi cha kwanza na sasa Yanga inafikisha pointi nne baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Lipuli ya Iringa kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, Dar es Salaam.

Yanga watakuwa wageni wa Maji Maji Jumamosi wiki hii Uwanja wa Maji Maji mjini katika mchezo wa tatu wa Ligi Kuu na wa pili mfululizo ugenini baada ya kuvuna pointi nne katika mechi zilizotangulia.

Katika mechi nyingine za VPL 2017/2018 Jana September 10,2017-; Lipuli FC imeilaza 1- 0 Stand United, Mbeya City imefungwa nyumbani 1-0 na Ndanda FC, Singida United imeifunga 2-1 Mbao FC, Kagera Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar imeshinda 1-0 dhidi ya FC Mwadui.

Post a Comment

0 Comments