habari Mpya


Taswira Picha Mbunge Msukuma na Madiwani Geita wamefunga barabara kisa Bilioni 26 wanazoidai Mgodi wa GGM.

Mbunge wa Jimbo la Geita mkoani Geita,Mhe.Joseph Kasheku Msukuma akiambatana na Madiwani wa Halmashauri zote za Mji na wilaya ya Geita pamoja na Wananchi wamefunga barabara ya kuingia mgodi wa dhahabu GGM,kukata bomba la maji na kuzingira uwanja wa ndege wa mgodi huo.

Mhe.Msukuma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani humo ameiambia Radio Kwizera kuwa lengo la zuio lao ni kushinikiza uongozi wa mgodi kuwalipa kiasi cha Dola za kimarekani milioni 12.65 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 26.

Mhe.Msukuma Amesema fedha hizo ni malimbikizo ya ushuru wa huduma tangu mwaka 2004 na kwamba kama zingetolewa kwa wakati zingeharakisha maendeleo ya mkoa wa Geita.


Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mtakuja Bw.Costantine Moorland kwa niaba ya madiwani wenzake amesema zuio hilo ni endelevu hadi uongozi wa GGM utakapohiari kulipa fedha zote.   

Post a Comment

0 Comments