habari Mpya


R.I.P Grand pa..Mfalme wa Muziki wa Country Duniani Don Williams.

Don Williams alianza kuimba muziki kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971.

Mwanamuziki nyota wa nyimbo za mtindo wa country kutoka Marekani Don Williams amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.

Mzaliwa huyo wa jimbo la Texas amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, afisa anayesimamia mawasiliano yake ametangaza.

Williams alianza kuimba nyimbo kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971, na tangu wakati huo alichomoa nyimbo 17 zilizogonga chati za muziki wa country.

Nyimbo zake zilizovuma zaidi ni pamoja na Gypsy Woman na Tulsa Time, ambazo ziliimbwa tena na wanamuziki wengine kama vile Eric Clapton na Pete Townshend. Williams alitazamwa na wengi kama gwiji mnyenyekevu wa muziki wa country.

Nyimbo zake nyingine zilizovuma ni pamoja na You're My Best Friend, I Believe in You na Lord, I Hope This Day Is Good.
Troy Gentry alikuwa amepangiwa kutumbuiza Medford Ijumaa jioni.

Mwanamuziki mwingine wa country kutoka Marekani Troy Gentry, pia amefariki, akiwa na miaka 50.

"Ni kwa huzuni kubwa ambapo tunathibitisha kwamba Troy Gentry, mmoja wa wanamuziki wawili wa country waliofahamika kama Montgomery Gentry amefariki katika akjali ya helikopta ambayo ilitokea mwendo wa saa saba mchana Medford, New Jersey," taarifa kwenye tovuti ya bendi hiyo ya wanamuziki wawili imesema.

Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika.

Wawili hao walikuwa wamepangiwa kutumbuiza Medford Ijumaa jioni.

Habari-BBC Swahili.

Post a Comment

0 Comments