habari Mpya


Radio Kwizera FM- Sakata la Mgodi wa GGM na Madiwani laingia Sura Mpya / Mbunge Msukuma ashikiliwa na Polisi.


SOURCE: RK, wm (Maralia)
ED: AG
DATE: Sunday, September 17, 2017

BUKOBA

Vifo vitokanavyo  na ugonjwa  wa Malaria  katika  halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera vimepungua kutoka watu  34 kwa  mwaka 2016 na kufikia watu 11katika kipindi cha mwaka 2017
Mganga mkuu wa manispaa ya Bukoba Dr. Hamza Mngula amesema hayo wakati akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Kijuu juu ya hali ya upatikanaji wa dawa za kutibu ugonjwa wa Malaria katika vituo vya afya na zahanati katika manispaa hiyo

Amesema kutokana na hamasa ya matumizi sahihi ya vyandaru pamoja na dawa inayoendelea kwa wakazi wa manispaa ya Bukoba, ndiko kumechangia kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kupungua  

Insert……..Dr Mngula
Cue in ……
Cue out …..

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Kijuu amesema juhudi za kutokomeza ugonjwa wa Malaria zinapaswa kuendelea hasa kuhimiza wananchi kufyeka vichaka jirani na vyumba zao sambamba na kutumia vyandarua nyakati za usiku 


SOURCE: RK, JJ (Msukuma akamatwa)
ED: AG
DATE: Sunday, September 17, 2017

GEITA
Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Msukuma kwa madai kuwa aliaandaa maandamano yaliyosababisha uharibifu wa miundombinu ya maji katika mgodi wa dhahabu GGM

Kamanda wa Polisi Mkoani humo Mponjoli Mwabulambo akizungumza na mwandishi wetu Juventus Juvenary amesema Mbunge huyo amekamatwa leo mchana na kwamba anaendelea kuhojiwa

Mbali na Mbunge huyo, madiwani wengine sita wote kutokana na Chama cha Mapinduzi CCM wanashikiliwa tangu juzi wakihusihwa na maandamano hayo 

Insert…Mponjoli
Cue In……….
Cue Out………

Ikumbukwe kuwa Mapema wiki iliyopita jeshi la Polisi mkoani Geita lililazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya maandamano ya madiwani pamoja na wananchi walioweka vizuizi katika barabara inayoingia mgodi wa dhahabu GGM wakishinikiza kulipwa ushuru wa huduma kiasi cha dola za kimarekani milioni 12.65.

SOURCE: RK, AG (Opareshi tokomeza uhalifu)


ED: AG

DATE: Sunday, September 17, 2017

NGARA


Jeshi la polisi wilayani Ngara mkoani Kagera linamshikilia mwanaume Justine Charles maarufu kama Sande mkazi wa kitongoji cha Matoketoke kata ya Ntobeye baada ya kukutwa na gunia 57 za bangi sawa na kilogram elfu 2 na 75 zikiwa zimehifadhiwa nyumbani kwake
Akizungumza na radio Kwizera akiwa makao makuu ya polisi Ngara, kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augostine Ollomi amesema mafanikio ya kukamata bangi hiyo yamekuja kufuatia oparesheni ya kutokomeza uhalifu iliyoanza Septemba 10 na kumalizika Septemba 16 mwaka huu ikihusisha mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita

Insert………Kamanda Ollomi
Cue In…………..
Cue Out……..

Akizungumza akiwa kituoni hapo mtuhumiwa huyo Justine Charles amesema licha ya kuwa ulimaji wa bangi ulipigwa marufuku na serikali lakini aliamua kuendelea kulima kutokana na ugumu wa maisha alionao ili ajipatie kipato

Kamanda Ollomi amesema katika oparesheni hiyo iliyofanyika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera pia wamefanikiwa kukamata kilogram 10 za mirungi, lita 527 za pombe aina ya Gongo, watu 25 wanaojihusisha na wizi, piki piki mbili,  Ng’ombe 16 waliokuwa wakisafirishwa pamoja na raia 60 wa kigeni walioingia nchini bila kufuata utaratibu


SOURCE: RK, Albert (WITO)

ED: AG

DATE: Sunday, September 17, 2017


KASULU

Askofu wa Jimbo katoliki la Kigoma muhasham Joseph Mlola amewataka waumini wa jimbo hilo kuwatoa vijana wao wa kike na kiume kujiunga na miito ya utawa na upadre ili kuendeleza utume wa kristo

Mhasham Mlola ametoa kauli hiyo jana katika sherehe za kuweka nadhiri za utume masista 18 wa shirika la Bene-Maria walipo katika kanisa la Petro mtume Murubona parokia ya Kasulu mjini

Amesema katika kutimiza agizo la kristo, wazazi hawana budi kuwafundisha watoto na kuwatoa kwa ajli ya kazi ya Mungu ya kuihubiri injili kwa mataifa 

Katika sherehe hizo Masista 13 wameweka nadhiri zao za kwanza, wanne wameweka nadhiri za milele na mmoja amefanya jubilei ya miaka 25 ya utume wake


SOURCE: RK, em (Kuugua magonjwa mbalimbali)

ED: AG

DATE: Sunday, September 17, 2017


KARAGWE

Wananchi wametakiwa kuwa na moyo wa kusamehe pale wanapokosewa ili kuepuka kuungua ugonjwa wa presha ambao pengine husababishwa na watu kuweka kinyongo moyoni kwa muda mrefu

Wito huo umetolewa leo na padre Juhudi Mosses wa kanisa la Mt. George jimbo katoliki la Kayanga wilayani Karagwe mkoani Kagera wakati akihubiri katika ibada ya misa takatifu 

Padre Mosses amesema kuwa duniani hakuna mtu mkamilifu hivyo ili kila mmoja aweze kupata msamaha kutoka kwa mwenyez Mungu anapaswa kusamehe kwanza wenzake 

Baadhi ya waumini ambao wamezungumza na radio kwizera mara baada ya ibada hiyo, wamesema ili mwanadamu aweze kutoa msamaha anatakiwa awe mtu mwenye hofu Mungu kwani kwa hali ya kibinadam inakuwa vigumu


SOURCE: RK, Elias Z (ardhi)

ED: AG

DATE: Sunday, September 17, 2017


CHATO

Serikali za vijiji katika kata mbalimbali wilayani Chato mkoani Geita zimetakiwa kuanza kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wakulima na wafugaji ili kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza baina yao

Akitoa agizo hilo mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Chato Mhandisi Joel Hali amesema kuwa watu na mifugo huongezeka kila siku hivyo serikali za vijiji kwa kushirikiana na madiwani wao hawana budi kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi

Kadhalika mhandisi Hali ameongeza kuwa halimashauri itawaagiza maafisa ugani walioko kila kata na vijiji kushirikiana na serikali za vijiji kupanga mikakati ya matumizi ya raslimali ardhi iliyopo

Insert……….Mkurugenzi
Cue in…………..
Cue out……………

Nae mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya Chato Bw Christian Manunga amewashauri wafugaji kuacha kufuga mifugo mingi kwenye eneo dogo badala yake wauze mifugo hiyo na kubuni miradi mingine ya kiujasilriamali


SOURCE: RK, AG (Salam za Shukrani)

ED: AG

DATE: Sunday, September 17, 2017


NGARA

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakt. John Magufuli ametuma salam za shukrani kwa Akofu wa jimbo katoliki la Rulenge Ngara kwa mapokezi mazuri aliyoyapata wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Ngara hivi karibuni.

Akiwasilisha salam hizo kwa waumini wa parokia ya Ngara mjini mara baada ya ibada ya misa takatifu, Muhashamu Askofu Severine Niwemugizi amesema rais alifurahishwa na namna alivyohudumiwa pamoja na mwenzake rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.

Askofu Niwemugizi amesema shukrani hizo alizozipata si za kanisa katoliki pekee bali ni kwa wilaya nzima ya Ngara na anawashukuru viongozi wa wilaya hiyo kwa kumpatia heshima ya kumuhifadhi rais.

Insert……….Niwemugizi
Cue In……….
Cue Out…….

Itakumbukwa kuwa Julai 20 mwaka huu rais Dakt John Magufuli alikutana na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa ziara ya kikazi wilayani Ngara na makao makuu ya uaskofu wa jimbo katoliki la Rulenge-Ngara ndipo palifanyika mazungumzo baina ya viongozi hao wawili.


SOURCE: RK, LT (Mauaji)

ED: AG

DATE: Sunday, September 17, 2017


KINSHASA
Mwakilishi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameitaka serikali ya nchi hiyo kuanzisha uchunguzi dhidi ya mauaji ya waomba hifazi 36 kutoka Burundi ambao wameuawa kwa kupigwa risasi na jeshi la DRC katika mji wa Kamanyola.

Kupitia tangazo lililotolewa na ofisi ya umoja wa mataifa nchini DRC, Bw Maman Sidikou ameonyesha masikitiko yake juu ya mauaji ya watu hao na kueleza kuwa jeshi halipaswi kutumia risasi za moto kwa ajili ya kutawanya waandamanaji mpaka kufikia kuuwa watu wengi kwa wakati moja.

Bw Sidikou amesema mauaji hayo ni miongoni mwa makosa ya jiniai hivyo ameomba mahakama ya kijeshi nchini DRC ifungue mashitaka dhidi ya maaskari waliohusika .

Siku ya Ijumaa mchana jeshi la DRC limewaua kwa kuwapiga risasi watu 36 na kujeruhi wangine 185 wote wakiwa waomba hifazi kutoka nchini Burundi baada ya wao kuvamia ofisi ya kitengo cha ujasusi kwa lengo la kuomba ndugu zao wanne waliokuwa wamezuiliwa waachiwe huru.

Post a Comment

0 Comments