habari Mpya


Prof. Ibrahim Hamis Juma Aapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Septemba, 2017 amemwapisha Prof. Ibrahim Juma kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akichukua nafasi ya Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Chande.

Uteuzi huo wa Jaji Mkuu wa Tanzania umeanza jana tarehe 10 Septemba, 2017.Kabla ya uteuzi huo Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amechukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Post a Comment

0 Comments