habari Mpya


Picha/Habari –Ziara ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini akiwa Mkoani Kagera.

Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini Dr Anna Peter Makakala akiwa wilayani Ngara,mkoani Kagera leo September 27,2017.

 Kamati  za ulinzi na usalama katika wilaya ya Ngara, Misenyi ,Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera  zimeagizwa kusitisha kupokea wakimbizi katika kambi za muda kwa raia wanaotoka nchi  jirani na  kwamba wageni watakaoingia sio wakimbizi bali watakuwa ni wahamiaji haramu.

 Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini Dr Anna Peter Makakala alitoa agizo hilo katika nyakati tofauti katika ziara ya kiutendaji mkoani Kagera jana na kwamba nchi wanakotoka wakimbizi hao kuna amani na utulivu hivyo warejee na kujenga nchi yao  kimaendeleo na kiuchumi.

Dr Makakala amesema katika mkoa wa Kagera unapakana na nchi ya Uganda Rwanda Burundi wananchi wasioe wanawake raia wa kigeni  kinyume na taratibu lazima walipiwe hati ya ukaazi  ambayo  ni kiasi cha Sh100 000 zinazolipiwa kupitia idara ya uhamiaji wala si kuwapatia viongozi katika serikali za vijiji.

"Fedha hizo zinalipwa kwa kipindi cha miaka miwili mara baada ya kukamilika mhusika anatakiwa alipie tena hivyo kuweni makini kufuata taratibu" Alisema Dr Makakala
 
Alisema wakimbizi wanaotoka nchini Burundi wanatakiwa kurejea kwenye nchi yaokufanya shughuli za maendeleo  na wasipokelewe kwenye kambi za muda zilizopo katika kata ya Bugarama na Murusagamba wilayani Ngara

Katika Kambi ya Bugarama wamekutwa raia 109 kutoka nchini Kongo DRC  waliotoka kambi za Burundi wakidai wamekimbia nchi yao kwa kukosa amani na katika kambi za Burundi zinakabiliwa na uhaba wa chakula ambapo Kamishna Jenerali Makakala amesema raia hao wamepoteza sifa ya kuwa wakimbizi 
 
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na idara ya uhamiaji ifanya taratibu za kuwarejesha hawa raia kwenye kambi zao licha ya kutambua kuwa DRC bado wanakabiliwa na changamoto za usalama kisiasa


Akizungumza na wafanyakazi wa idara ya uhamiaji mjini Ngara na Kabanga Dr Makakala aliwataka watumishi wa idara hiyo kufanya kazi kwa uadilifu kwa kujiepusha na vitendo cha rushwa na kuhudumia wananchi bila upendeleo huku akisisitiza ushirikiano na watendaji wa idara hiyo kutoka nchi jirani.

Akiwa katika kituo cha forodha Kobero mpakani mwa Tanzania na Burundi aliwataka  madereva wa magari  wanaokwenda nchi za jirani kuhakikisha wanatumia paspoti kuingia katika mataifa ya kigeni  kuepuka usumbufu unaoweza kuwakumba katika shughuli zao.

Pia aliahidi kuongeza watumishi wa idara ya uhamiaji mkoani Kagera na kwamba ataiomba serikali isaidie  kutoa vifaa  vya kufanikisha utendaji kazi wa idara ya uhamiaji vikiwemo vyombo vya usafiri kukabiliana na wimbi la kudhibiti wageni sehemu zote za mipakani kote nchini.

Naye  msemaji mkuu wa idara ya uhamiaji Ally Mtanda alisema kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu Idara hiyo mkoani Kagera kwa kushirikiana na jeshi la polisi   imekamata raia wa kigeni 2,426 kutoka mataifa mbalimbali ambapo waliorudishwa katika mataifa yao ni 1,790.

Alisema pia takwimu za kitaifa ni kwamba raia 141,639 waliingia nchini kati ya hao watanzania ni 67, 318 na  wageni ni 74,321 ambapo  wageni waliotoka Tanzania kwenda mataifa ya nje ni 139,091 kati ya hao watanzania ni  73,738 na raia wa kigeni ni 65,353 kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa kisheria.

Awali mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni kanali Michael Mntenjele akitoa taarifa ya wilaya hiyo   kuhusu raia wa kigeni wanaoingia wilayani huno amesema wilaya hiyo inao waomba hifadhi 223 kutoka Burundi na DRC ambao wanapokelewa katika kambi ya Rumasi wilayani Ngara

Alisema changamoto maeneo ya mipakayao wazi na kutokuwepo askari wa kutosha kila mpaka kudhibiti RAIA wa kigeni ambao huingia kifanya kazi kwa watanzania baadhi hupata makazi na wengine kuolewa

Pia alisema vigingi vya mipaka vilivyowekwa tangu ukoloni na vingine vya mwaka 2014 chini ya rais jk na Nkurunziza vinaingia kwenye mashamba ya wananchi na kwamba walioolewa au kuoa wanakabiliwa na ukosefu wa fedha dola 50 za kulipia hati ya ufuasi.

Post a Comment

0 Comments