habari Mpya


Jeshi la Polisi Ngara lakamata Magunia 57 za Bangi nyumbani kwa Justine Charles maarufu Sande.

Justine Charles akiwa amekamatwa na shehena ya Madawa ya kulevya aina ya Bangi magunia 37 huko nyumbani kwake Mkatokatoke kijiji cha Ntobeye wilayani Ngara mkoani Kagera tarehe 15,09,2017.

Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera linamshikilia  Justine Charles maarufu kama Sande mkazi wa kitongoji cha Matoketoke kata ya Ntobeye baada ya kukutwa na gunia 57 za bangi sawa na kilogram elfu 2 na 75 zikiwa zimehifadhiwa nyumbani kwake.

Akizungumza na Radio Kwizera akiwa Makao Makuu ya Polisi Ngara, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Augostine Ollomi amesema mafanikio ya kukamata bangi hiyo yamekuja kufuatia oparesheni ya kutokomeza uhalifu iliyoanza Septemba 10 na kumalizika Septemba 16 mwaka huu,2017 ikihusisha mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Akizungumza akiwa kituoni hapo mtuhumiwa huyo Justine Charles -Pichani amesema licha ya kuwa ulimaji wa bangi ulipigwa marufuku na serikali lakini aliamua kuendelea kulima kutokana na ugumu wa maisha alionao ili ajipatie kipato.

 Kamanda Ollomi amesema katika oparesheni hiyo iliyofanyika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera pia wamefanikiwa kukamata kilogram 10 za mirungi, lita 527 za pombe aina ya Gongo, watu 25 wanaojihusisha na wizi, piki piki mbili,  Ng’ombe 16 waliokuwa wakisafirishwa pamoja na raia 60 wa kigeni walioingia nchini bila kufuata utaratibu.

Post a Comment

0 Comments