Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
imetangaza ajira za walimu wa shule za msingi kwa walimu ambao wamemaliza
masomo yao mwaka 2014/2015 katika ngazi ya cheti (III A).
Taarifa
iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na
kuthibitishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas imesema kuwa walimu
ambao wamemaliza mwaka 2014/2015 na walituma maombi yao kwenye tangazo la kazi
ya Agust 10, 2017 hawatakiwa kuomba upya kwani barua zao zinafanyiwa kazi.
|
0 Comments