habari Mpya


David Luis alambwa Red Card wakati Chelsea na Arsenal Hakuna Mbabe.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Chelsea wamelazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa vuta nikuvute uliochezwa Stamford Bridge.

Tukio kubwa zaidi kwenye mchezo huo, ni kupewa kadi nyekundu kwa beki wa Chelsea David Luis kunako dakika ya 86 baada ya kumchezea rafu beki tatu wa Arsenal Sead Kolasinac.

Baadhi ya wachambuzi wakiwemo Alan Shearer na Peter Schmeichel wamepata kigugumizi juu ya kadi hiyo nyekundu huku wengi wao wakiamini kadi njano ingekuwa uamuzi sahihi.

Mchezo huo uliojaa ufundi wa kila namna, pia ulitawaliwa na ubabe mwingi na kumpelekea mwamuzi Michael Oliver kutoka kadi za njano mbili kwa Chelsea na tatu kwa Arsenal.Post a Comment

0 Comments