habari Mpya


Mwenge wa Uhuru 2017 Kuanza Mbio zake mkoani Kagera.

Mwenge wa Uhuru unatarajia kuingia Mkoani Kagera leo August 1, 2017 ukitokea Mkoani Kigoma ambapo utaanza kukimbizwa wilaya ya Biharamulo na kupitia miradi 7 ya kimaendeleo yenye thamani ya Tsh1.226 Bilioni.

Ukiwa wilayani Ngara,Mwenge wa Uhuru utapitia miradi 11 ya Maendeleo yenye thamani ya Tsh4.5 Bilioni kabla ya kuingia wilaya ya Karagwe, Kyerwa, Misenyi, Bukoba Halmashauri, Bukoba  Manispaa na kuhitimisha mbio zake Kimkoa wilayani Muleba.

Post a Comment

0 Comments