habari Mpya


Rais Magufuli awasili Mkoa wa Mwanza kuzindua Mradi wa Maji July 04, Sengerema.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.

Rais John Magufuli anazindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema hapo Leo July 04,2017.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Bw.Emmanuel Kipole amesema kuwa Rais Magufuli atafika Wilayani hapo kwa ajili ya uzinduzi huo.

Mradi huo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2014 kwa gharama ya Sh bilioni 23 utawanufaisha zaidi ya wakazi wa wilaya hiyo 13,000 ambapo amesema wilaya hiyo ina jumla ya wakazi 74,186 kutokana na Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2002 hivyo mradi huo kwa sasa utahudumia kata 11.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono washabiki waliohudhuria mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wachezaji wa Buhongwa Fc mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana.

Post a Comment

0 Comments