habari Mpya


Matukio Picha Wana RK –Ngara walivyosheherekea Sikukuu ya Mt. Inyasi wa Loyola.

Anayekata keki ni Fr.Damas Missanga SJ Mkurugenzi wa Radio Kwizera sambamba na Br. Deus SJ wakifurahia keki na Mis Auleria Gabriel kulia ,Kanyesha Faustine ,Amina Semagogwa na Paschal Mwaliyenga wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya Mt Inyasi wa Loyola leo Julai 31,2017 nje ya Ofisi ya Radio Kwizera ,Ngara,Kagera.
 
Akizungumza na Mtandao huu wa Radiokwizerafm  ,Mkurugenzi wa Radio Kwizera,Fr.Damas Missanga SJ amesema kuwa Siku hii iliyo kuu (twaiadhimisha) tunaiadhimisha  kwa heshima yake (Mtakatifu) Inyasi wa Loyola ,Tunasherehekea sote, nyuso zimejawa furaha kwa sababu Alijitoa kwa moyo weke bila ya kujibakiza,kuleta mabadiliko tele katika maisha ya kiroho na ya sisi wakosefu.
 Fr.Missanga SJ amewataka Wafanyakazi wa Radio Kwizera  tuuige  mfano huo bora aliyotuonyesha Mtakatifu (Mt. Inyasi wa Loyola)  ,alivyodhihirisha upendo wake, kwake Mungu Baba.


Mtakatifu Inyasi wa Loyola alizaliwa mwaka 1491 huko Loyola, Guipúzcoa, Hispania akafariki tarehe 31 Julai 1556, mjini Roma (leo nchini Italia).
 
Alikuwa Padri wa Kanisa Katoliki maarufu hasa kama mwanzilishi wa Shirika la Yesu na wa mtindo wa mazoezi ya kiroho.
Alitangazwa na Papa Paulo V kuwa mwenye heri tarehe 27 Julai 1609, halafu Papa Gregori XV alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Machi 1622.
 
 
 Kutokana na heshima yake jina lake ni jina la shule iliyopo Mabibo, Dar es salaam nchini Tanzania.
 
HAPA CHINI NI MATUKIO PICHA WAKATI WA KEKI IKIKATWA KISHA KULIWA.
Pozi la keki ,wa kwanza ni Mwana wa Makonda sambamba na Br. Deus SJ  ,Kanyesha Faustine ,Amina Semagogwa na  Fr.Damas Missanga SJ Mkurugenzi wa Radio Kwizera  wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya Mt Inyasi wa Loyola leo Julai 31,2017 nje ya Ofisi ya Radio Kwizera ,Ngara,Kagera.

Wa kwanza kushoto Laurent Gervas,Mwana wa Makonda ,Amina Semagogwa,Kanyesha Faustine na Godwin Bruchard wakifurahia pozi la picha na keki wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya Mt Inyasi wa Loyola leo Julai 31,2017 nje ya Ofisi ya Radio Kwizera ,Ngara,Kagera.


Mwana wa Makonda ,Amina Semagogwa na Kanyesha Faustine wakifurahia pozi la picha na keki wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya Mt Inyasi wa Loyola leo Julai 31,2017 nje ya Ofisi ya Radio Kwizera ,Ngara,Kagera.


Mis Amina Semagogwa katikati , Kanyesha Faustine na Auleria Gabriel kulia wakifurahia pozi la picha na keki wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya Mt Inyasi wa Loyola leo Julai 31,2017 nje ya Ofisi ya Radio Kwizera ,Ngara,Kagera.


Mwana wa Makonda kushoto na Boaz Zobanya walifumwa na Camera wakitafuna keki kwenye pozi la picha  wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya Mt Inyasi wa Loyola leo Julai 31,2017 nje ya Ofisi ya Radio Kwizera ,Ngara,Kagera.

Mwana wa Makonda ,Amina Semagogwa,Kanyesha Faustine na Godwin Bruchard wakifurahia pozi la picha na keki wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya Mt Inyasi wa Loyola leo Julai 31,2017 nje ya Ofisi ya Radio Kwizera ,Ngara,Kagera.

Post a Comment

0 Comments