habari Mpya


Je Serikali hamuioni Barabara Kuu Nyakanazi hadi Rusumo inavyotesa Wasafiri na Magari.??

Hali ya barabara kuu Nyakanazi -Rusumo hapa eneo la Nyabugombe linavyoonekana bovu kwa kujaa mashimo makubwa yasiyopitika kwa urahisi.

Zaidi ya magari 100 ya Abiria na Mizigo Jana July 11, 2017  yamekwama kwa muda kuendelea na safari yakitoka Jijijini Dar es salaam na Mikoa mingine kuelekea Nchi za Burundi na Rwanda Eneo la Nyabugombe mpakani mwa wilaya ya Biharamulo na Ngara mkoani Kagera katika barabara kuu ya Nyakanazi – Benaco kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

Hata hivyo hali imekuwa ngumu zaidi kwa wasafiri wanaoitumia barabara hiyo ambao wakizungumza bila matumaini ya kuboreshwa kwa barabara hiyo kuu eneo la tukio, wameelezea mazingira magumu yanayowakabili katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kukosa huduma za msingi kama chakula na mawasiliano ya simu kutokana na eneo hilo kukosa network.

Hapa Kutaga kwa sana ,Magari hayo yamekwama kwa kuharibika au kushindwa kupita baada ya barabara kuzibwa na magari yaliyokwama.

Wakizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu, Baadhi ya Madereva  waliokwama hapo wamesema kuwa kukwama kwao ni kutokana na ubovu wa barabara  ambao umesababisha mashimo makubwa licha ya kila wakati wote barabara hiyo kuwa katika matengezo ambayo  wamesema kuwa yapo chini ya kiwango.

Barabara Kuu ya Nyakanazi hadi Rusumo kwa muda mrefu sasa imekuwa korofi kutokana na kukosekana kwa matengenezo ya uhakika katika barabara hiyo muhimu kibiashara kati ya nchi za Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi.
Udongo wenye vumbi unavyoonekana huku ukiyafunika mashimo  makubwa makubwa licha ya kila wakati wote barabara hiyo kuwa katika matengezo ambayo yanaelezwa na watumiaji wa barabara hiyo kuwa yapo chini ya kiwango.

 
Kujikwamua kupita mashimo mpaka tairi jipya kabisa lililofungwa garini  linaharibika


Post a Comment

0 Comments