habari Mpya


HOTUBA-Rais Magufuli katika Uzinduzi Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato Kielektroniki (Data Centre) 01 June,2017 .

Rais Magufuli akizindua mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki akishuhudiwa na Rais wa SMZ, Dkt. Shein na VP Samia Suluhu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Jana Alhamisi, Juni 1, 2017 amezindua rasmi Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa njia ya Kielektroniki.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa serikali wakiwemo Rais wa Zanzibar, Dkt. Ally Mohammed Shein, Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na wengine, Rais Magufuli alianza kukagua Kituo cha Taifa cha Kutunzia Taarifa (Data Center), kilichopo TTCL Kijitonyama na kuridhishwa na mafanikio makubwa ya ubunifu huo.

Bofya Play hapa chini kusikiliza yote aliyoyasema na Rais Magufuli.

Post a Comment

0 Comments