habari Mpya


COSAFA Castle Cup 2017- Tanzania Kinara Kundi A kufuzu ikiifunga Mauritius Alhamisi.

Tanzania Jana ilitoka Sare 0-0 katika Mechi yake ya Pili ya Kundi A ya Mashindano ya COSAFA Castle Cup 2017 dhidi ya Angola iliyochezwa huko Royal Bafokeng, Rustenburg, Afrika Kusini.

Hii ni Mechi ya pili kwa Tanzania baada ya kuichapa Malawi 2-0 katika Mechi yao ya kwanza na inawafanya kuongoza Kundi A wakiwa na Pointi 4 wakifuata Angola wenye 4 pia huku Mauritius na Malawi zikiwa mkiani zikiwa na Pointi 1 kila mmoja baada ya mapema Jana kutoka 0-0.

Tanzania itacheza Mechi yake ya mwisho ya Kundi A dhidi ya Mauritius hapo Alhamisi huko Moruleng.

Mshindi wa Kundi A atakipiga na South Africa kwenye Robo Fainali.
FAHAMU:

Hii ni mara ya 3 kwa Tanzania kucheza Mashindano haya baada ya kushiriki yale ya 1997 na 2015.

Kundi B la Mashindano la 2017 COSAFA Castle Cup lina Nchi za Zimbabwe, Madagascar, Mozambique na Seychelles.

Nchi Wanachama wa COSAFA, South Africa, Swaziland, Botswana na Zambia wataanzia Hatua ya Robo Fainali ambapo South Africa itacheza na Mshindi wa Kundi A na Swaziland kucheza na Mshindi wa Kundi B wakati Botswana ikivaana na Zambia.

Mashindano ya COSAFA yalianzishwa Mwaka 1997 na Nchi za South Africa, Zambia na Zimbabwe kubeba Kombe mara 4 kila moja wakati Angola ikibeba mara 3 na Namibia mara 1.

Post a Comment

0 Comments