habari Mpya


Alhaj Bulembo -Awavuta 71 CCM akiwemo Ninian Bakari kutoka Chadema wilaya ya Ngara.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM , Alhaj Abdallah Bulembo akipokea kadia kutoka kwa Bi.Niniani Bakhari, aliyekuwa Kada machachari wa CHADEMA wilaya ya Ngara mkoani Kagera, ambaye alitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa ndani uliofayika Jana June 5,2017 katika mji mdogo wa Ngara mkoani Kagera.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimpongeza Ninian kwa uamuzi wake wa kurejea CCM.
Baadhi washiriki wa kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ngara,mkoani Kagera, Mabalozi na Viongozi kutoka Jumuia zote za CCM wakimpongeza Bi.Ninian Bakari kwa furaha baada ya kukabidhi kadi yake ya CHADEMA alikohamia mwaka 2015 kwa Alhaj Bulembo wakati wa kikao hicho.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisikiliza kwa makini wakati Bi.Ninian Bakari alipokuwa akieleza yake ya moyoni, alisema aliamua kwenda CHADEMA  baada ya kuona CCM ya wakati huo ina mambo mengi ya hovyo, lakini sasa ameamua kurejea baada ya kuona kuwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli amekisafika Chama.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abadalla akitoa kadi kwa mmoja wa wanachama hao wapya 71 waliohamia CCM wakati wa kikao hicho.
 
Wengine waliamua kumkabidhi Alhaj Bulembo hadi bendera ya CHADEMA baada ya kulifunga tawi lao.
 
Baadhi ya kadi za CHADEMA zilizorejeshwa kwa Alhaj Bulembo.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo (kushoto) akishiriki wakati wachama wapya 71waliohamia CCM wakitokea Chadema, walipokuwa wakila kiapocha Mwana CCM, baada ya kukabidhiwa kadi za Chama kwenye kikao hicho,hapo Jana June 5,2017.
 
Ukumbi ukilipuka kwa nderemo na vifijo baada ya wanachama hao wapya kulakiapo.
 
Wajumbe wakiwa ukumbini kuendelea na kikao baada ya zoezi hilo la kupokea wanachama wapya 71 wa CCM kutoka CHADEMA.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kagera, Mhe.Oliva Semgurika akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho.
 
Mwenyekitiwa CCM wilaya ya Ngara Hudson Bagege akifunguakikao hicho. Kulia kwake ni  Alhaj Bulembo.
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, Bi. Constansia Buhiye akimkaribisha Alhaj Bulembo kuzungumza katika kikao hicho.
 
Mzee Said Ramadhani Sudi akimkabidhi zawadi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo kabla ya kuzungumza katika kikao hicho.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya mapokezi Mzee Jason Bahemu akikabidhi zawadi maalum ya kimila kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya  CCM Alhaji Abdallah Bulembo kabla ya kuzungumza katika kikao hicho.
 
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Alhajj Abdallah Bulembo akizungumz na Wajumbe wakati wa kikao hicho cha Wajumbe wa wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ngara, Mabalozi, Viongozi wa Jumuia zote za CCM na watendaji wa Serikali.
 
Vijana wa UVCCM wakimvisha skafu mjumbea wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdalla Bulembo wakati wa mapokezi kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Jana June 5,2017.
 
Vijanawa UVCCM wakionyesha ukakamavu wao wakati wa paredi la mapokezi.

Vijana wa UVCCM na Skauti wakifanya manjonjo yao ilimradi kunogesha mapokezi ya Mjumbea wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulebo alipowasili Ofis ya CCM Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Jana June 5,2017.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia baadhi ya viongozi alipowasili kweneye Ofisi ya CCM Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Jana June 5,2017. 
Kushoto ni Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Bi.Mwajemi Balagama.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwa na viongozi wengine meza kuu alipowasili ukumbini baada ya kutoka Ofisi ya CCM Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Hapo Jana June 5,2017.
 
Mjumbe wa NEC Ngara, Issa Saama akisalimia baada ya kutambulishwa.
Wazee maarufu walioalikwa kwenye kikao hicho wakiwa Ukumbini. 
PICHA: BASHIR NKOROMO

Post a Comment

0 Comments