habari


Wilaya ya Ngara mkoani Kagera yapokea Madawati 537 toka Mfuko wa Jimbo ili kutatua tatizo la Upungufu.

 Wazazi na Wanafunzi , shule ya msingi Mumiterama kata ya Nyamiaga -Picha toka Maktaba yetu.

Jumla ya shule za msingi 25 za wilaya ya Ngara mkoani Kagera zimepokea madawati kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngara ambayo yametolewa na mfuko wa jimbo ili kuondoa tatizo la upungufu wa madawati.

Afisa Elimu wa wilaya ya Ngara , Bw Gidion Mwesigwa amebainisha kuwa madawati yaliyotolewa kwa wilaya ya Ngara ni 537 ambayo tayari yameshaanza kusambazwa. 

Amesema shule zitakazopata madawati hayo ni shule mpya, shule zenye vyumba vya kutosha vya madarasa na shule ambazo zimepokea wanafunzi wengi wa elimu ya awali kwa mwaka huu.
Bw Mwesigwa pia ameishukuru kampuni ya Kabanga Nickel kwa mchango wao wa kujenga vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo na kuwataka wananchi kujitolea kwa wingi kuweka nguvu kazi zao katika kujenga shule

Post a Comment