habari Mpya


Watoto milioni 1.4 wana utapiamlo Somalia-UNICEF.

Shirika la Watoto Duniani (UNICEF), limesema kuwa watoto wasiopungua milioni 1.4 wana utapiamlo mkali ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 kulinganisha na mwaka uliopita.

Hayo yamebainishwa na muwakilishi wa UNICEF nchini Somalia, Steven Lauwerier, akisema kuwa hali hiyo ipo kwa sasa katika taifa hilo, na kuwa hali ni mbaya sana, hivyo kunahitajika msaada wa haraka ilikuweza kunusuru maisha ya watoto hao.

 Wananchi wa Somalia wamekuwa na kipindi kigumu kutokana na hali ya maisha nchini humo kuwa ngumu, wakikabiliwa na ukame wa muda mrefu, hali iliyosababisha wananchi wanaokadiriwa kufikia 615,000 kukimbia makazi yao.

Post a Comment

0 Comments