habari Mpya


Taswira Picha ya Ambulance 3 zilizotolewa na Rais Magufuli kwa Wabunge wa Majimbo ya Nkasi, Shinyanga na Tabora.

Mbunge wa Viti maalumu Tabora, Mhe. Munde Tambwe akifurahi baada ya kukabidhiwa gari hilo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa magari mapya matatu ya kubebea wagonjwa  (Ambulance) kwa Wabunge wa majimbo ya Nkasi, Shinyanga na Tabora ili kuwasaidia Wananchi wa maeneo yao ya Ubunge.
Wabunge hao wakielekea mahali ambapo magari hayo yalikuwa yameegeshwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amekabidhi magari hayo aina ya Land Cruiser Hardtop kwa niaba ya Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mkoa wa Rukwa Mhe. Ally Keissy, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa waTabora Mhe. Munde Tambwe na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga.
Mbunge wa viti maalum CCM, Lucy Mayenga akikabidhiwa funguo za gari na Balozi John Kijazi.
Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Kessy akifurahia baada ya kukabidhiwa gari hilo.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Balozi Kijazi amesema Mhe. Rais Magufuli ametoa magari hayo baada ya kuguswa na kilio cha muda mrefu cha Wabunge hao waliokuwa wakiomba wananchi wao wapatiwe magari ya wagonjwa.

Mhe. Rais ameamua kuwakabidhi nyinyi haya magari kutokana na vilio vyenu ambavyo amekuwa akivisikia mara kwa mara, Mhe. Keissy umekuwa hata ukitafuta miadi ya kuja kumuona Mhe. Rais kwa suala hili, Waheshimiwa Wabunge wamekuwa wakiyazungumza haya kwa muda mrefu.

Tunafahamu kila Mbunge katika jimbo lake anahitaji kupata huduma kama hii, na huduma kama hii ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, kwa hiyo sisi Serikali kila tunapopata uwezo basi tunasaidia pale tunapoweza kufikia kwa wakati ule, tulishatoa magari mengine matatu kama haya Chalinze na vituo vingine vya Morogoro.” Amesema Balozi Kijazi.

Taarifa Kamili ya Ikulu,soma hapa Chini.

Post a Comment

0 Comments