habari Mpya


Soma Taarifa ya Habari ya Saa SITA Mchana Leo May 24,2017-Radio Kwizera FM-Ngara.

TAARIFA KAMILI.

SOURCE: RK, KM (Wito)
ED: AG
DATE: Wednesday, May 24, 2017

KASULU.

Wanafunzi wa shule za wakimbizi raia wa Burundi kambini Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameombwa kuzingatia usafi wawapo shuleni ili kujikinga na magonjwa ya miripuko kambini humo.

Wito huo umetolewa na afisa afya kutoka shirika la Oxfam kambini Nyarugusu Bw Nicolas Charles akizungumuza wakati wa ziara yake katika shule za wakimbizi raia wa Burundi kambini humo

Bw Charlas ameeleza kuwa awali waligawa vyombo vya usafi shuleni lakini wengi wao wamekuwa hawazingatii taratibu za usafi

Katika ziara yake afisa afya ametowa msaada wa sabuni za usafi, sabuni za kuogea, mswaki na dawa ya meno na kuwaomba wanafunzi waliopewa vifaa hivyo kuvitumia kwa malengo yalio kusudiwa

SOURCE: RK, EM (Muuza madawa ya kulevya kukamatwa)
ED: AG
DATE: Wednesday, May 24, 2017

KARAGWE.

Mtu mmoja mkazi wa Kayanga wilayani Karagwe mkoani Kagera anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Adhibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Karagwe Bw Mika Makanja amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Peleusi Mishaki mwenye umri wa miaka 39

Bw Makanja amesema kuwa mtuhumiwa huyo amemkamatwa hivi karibuni akiwa katika maeneo ya mji mdogo wa Kayanga akiwa na misokoto 78 ya bangi akielekea kuuza

Insert…………Bw Makanja
Cue in…………..Tulimukamata
 Cue Out…………madawa

Hata hivyo amewataka wananchi wilayani Karagwe kuacha tabia ya kulima na kuuza dawa za kulevya kwa sababu biashara hiyo itawaletea matatizo badala yake walime na kuuza mazao ambayo ni halali kama vile Maharagwe, Viazi pamoja na Mahindi

SOURCE: RK, WM (Muuza madawa ya kulevya kukamatwa)
ED: AG
DATE: Wednesday, May 24, 2017.

BUKOBA

Wazazi na walezi mkoani Kagera wametakiwa kuunga mkono utoaji wa dawa za minyoo na kichocho kwa watoto wao kwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao  ili  kufanikisha adhima ya  serikali ya kukabiliana na magonjwa hayo

Kaimu afisa afya wa mkoa Kagera  Bw Gras Ishengoma ametoa wito huo wakati wa kikao cha kujadili kuhusu tahadhali ya ugonjwa wa  Ebola na utoaji wa dawa hizo kwa watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 14 kikao ambacho kimefanyika  katika ukumbi wa mkuu wa mkoa

Amesema kuwa magonjwa ya minyoo na tumbo bado yako juu ambapo utafiti uliofanyika mwaka 2016 katika halmashauri 4 ambapo shule ya msingi Kasozibakaya iliyopo halmashauri ya Biharamulo imeongoza kwa asilimia 82 ikifuatiwa na shule ya msingi Ibuga iliyopo wilayani Ngara kwa asilimia 71

Kwa upande wake afisa mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi  kipaumbele  kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto  Bw  Osca  Kaitaba amesisitiza  wazazi na walezi mkoani Kagera kuhakikisha wanatoa chakula kwa watoto.

SOURCE: RK, KK (Ebora)
ED: AG
DATE: Wednesday, May 24, 2017

MWANZA 

Mkoa wa Mwanza Bw John Mongela amesema kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa yenye uwezo mkubwa wa kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ebola ikiwa tahadhari haitachukuliwa mapema

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao Maalumu cha kujadili namna ya kukabiliana na kuchukua tahadhali ya maambukizi ya ugonjwa huo, Bw Mongela ameema tayari mkoa huo umechukua tahadhari za kukabiliana nao

Mongela amesema kuwa uwezekano wa mkoa wa Mwanza kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ebola  ni kutokana na kuwa kitovu cha biashara kwa nchi za ukanda wa maziwa makuu hivyo juhudi za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa ikiwa ni sambamba na utoaji wa elimu kwa wananchi

Insert…………Mongera
Ceuin…………
Ceout…………..

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr Leonard Suby amesema kuwa Tanzania katika historia yake haijawahi kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola hivyo ni muhimu kuchukua tahadhali ya kukabiliana na ugonjwa huo

Kikao hicho kimewashirikishaa wakuu wa wilaya za jiji la Mwanza, wakurugenzi, viongozi wa dini,waganga wakuu wa wilaya, mkurugenzi wa utafiti wa magonjwa ya Binadamu na viongozi wa ulinzi na usalama


SOURCE: RK, JJ (Kufa maji)
ED: AG
DATE: Wednesday, May 24, 2017

GEITA

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ameagiza halmashauri ya Wilaya ya Geita pamoja na wananchi wa kijiji cha Butwa kuweka ushirikiano ili kujenga shule kwenye kijiji hicho

Hayo ameyasema wakati akitoa pole kwa wafiwa na jamii ya Kitongoji cha Lulegea Kata ya Izumacheli kutokana na tukio la wanafunzi watatu wa shule ya msingi Butwa kufariki wakitokea shuleni kwenda Nyumbani

Kyunga amesema kuwa ili kuwasaidia wananchi wa Kitongoji cha Lulegea ni vyema wananchi kujumuika kwa pamoja na kushirikiana ili waweze kujenga shule ambayo itawasaidia wananfunzi

Bw Tululaza Kurulaenda ambaye alikuwa amewabeba wanafunzi hao kwenye Mtumbwi ambao umezama ameelezea kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na watoto kutokutulia wakati akiendesha Mtumbwi pamoja na hali ya ziwani kutokuwa shwali 

Hapo jana wanafunzi 24 wamezama maji ambapo watatu wamefariki wakitokea shule ya msingi Butwa iliyopo Kata ya Izumacheli na tayari miili ya watoto hao imezikwa kwenye kitongoji cha Lulegea

SOURCE: Ikulu, AG (Rpoti)
ED: AG
DATE: Wednesday, May 24, 2017

DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli amevunja bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania TMAA na kuagiza iweze kuchunguzwa

Rais Magufuli amefikia hatua hiyo hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ripoti ya Madini Katika Makontena ya Mchanga kutoka Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini (MAKINIKIA) yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini

Pia amemtaka waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospiter Muhongo kujitathmini na ikiwezekana aachie wadhifa huo kutokana na kushindwa kusimami kikamilifu wizara yake na kupelekea mchanga mwingi wa dhahabu kwenye makontena kuuzwa nje ya nchi

Insert………Magufuli
Cue In
Cue Out

Akiwasilisha ripoti hiyo mwenyekiti wa kamati ya wataalamu wa jiolojia na uchambuzi wa kisayansi iliyoundwa Machi 29 mwaka Prof Mruma amesema uchunguzi huo umebaini uwepo wa madini ya kiasi cha kati ya Shilingi bilioni 829.4 mpaka 1.439 Trillion kwa makontena 277

Insert………Prof Mruma
Cue In….
Cue Out

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Wasiliana/News Desk, Ngara Kagera.
Chief News Editor
Ms AuleriaGabriel
auleria@radiokwizera.com
Mobile: +255 769722554

Post a Comment

0 Comments