habari Mpya


Soma Habari ya Leo May 12,2017 -Saa 6 Mchana-Radio Kwizera FM-Ngara/Kagera.

Ms.Auleria Gabriel- Msomaji Leo May 12, 2017.

Wasiliana/News Desk, Ngara Kagera.
Chief News Editor
Ms AuleriaGabriel
auleria@radiokwizera.com
Mobile: +255 769722554   
                           
        HABARI KAMILI


SOURCE: RK, Gmika (siku 10)
ED: AG
DATE: Friday, May 12, 2017

BUKOMBE 

Jamii wilayani Bukombe Mkoani Geita imetakiwa kushirikiana kwa pamoja kumtafuta mtoto Mshauri Juma mwenye umri wa miezi sita aliyeibiwa nyumbani kwa mama yake na mwanamke ambaye hajafahamikana siku kumi zilizopita

Akizungumza na radio kwizera mwenyekiti wa mtaa wa shina la Kapera Adamu Kahorwe amesema hadi sasa hatma ya mtoto huyo bado haijajulikana kutokana na kutafutwa kwa muda mrefu bila mafanikio

Bw Kahorwe ameitaka jamii kushirikiana na wazazi wa mtoto huyo katika kumtafuta sehemu mbalimbali ndani na nje ya wilaya

Insert ……..Kahorwe
Cue in…….
Cue out…….

Bibi wa mtoto huyo Taabu Idika ameiomba serikali wilayani Bukombe kuwasaidia katika upelelezi ili kuweza kumkamata mwizi wa mtoto huyo


SOURCE: RK, ak [uchangiaji maji]
ED: AG
DATE: Friday, May 12, 2017

MISSENYI

Kutokana na wananchi wilayani Missenyi mkoani Kagera kushindwa kuchangia gharama za maji imesababisha baadhi ya miradi ya maji kukwama

Akizungumza na wadau wa maendeleo wilayani Missenyi, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw Limbe Moris amesema kuwa pale serikali inapoamua kujenga miradi ya maji na kuikabidhi kwa wananchi ni sharti wananchi wachangie fedha kwa ajili ya uendeshaji

Amesema kuwa hali hiyo imekuwa tofauti kwa wakazi wa Missenyi kwani asilimia kubwa ya wakazi wamekuwa wagumu kuchangia gharama za uendeshaji wa miradi ambapo amesema kuna haja ya kuwahamasisha wananchi kuchangia.

Insert.........limbe moris
Cue in......mwitikio mdogo
Cue out......na kuisimamia

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo akiwemo Asimwe Obadia na Paulo Julian wasema kuwa wananchi wamekuwa na ushiriki mdogo katika kuchangia kutokana na uhamasishaji mdogo kutoka kwa viongozi waliopewa jukumu la kusimamia

SOURCE: RK, Elias Z(baraza madiwani)
ED: AG
DATE: Friday, May 12, 2017

CHATO

Halimashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita imesema itawafungia wachimbaji wadogowadogo wenye migodi ya dhahabu ndani ya wilaya hiyo endapo wataendelea kukwepa kuchangia mapato ya halimashauri hiyo

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya ya Chato Bw Christian Manunga katika kikao cha baraza la madiwani ambapo amesema kuwa ni jambo la kushangaza kwani tangu migodi hiyo imeanzishwa hakuna kiwango chochote cha fedha ambacho kimeshalipwa ndani ya halimashauri 

Nae katibu wa wachimbaji wadogowadogo wilayani humo Bw Johnson Mnandu amabaye pia ni diwani wa kata ya Muungano amesema kuwa hakuna haja ya kuwafungia shuguli ya uchimbaji na badala yake atajitahidi kuwahamasisha na kuwaelimisha wenzake ili waweze kuichangia  mapato ndani ya halimashauri.

Insert……………..KATIBU WACHIMBAJI
Cuein………………….
Cueout………………..

Katika hatua nyingine Bw Mnandu ameiomba halimashauri kuwa na subira wakati wakiendelea kutekeleza agizo hilo la kuchangia mapato yatokanayo na migodi.

SOURCE: RK, sy (wazee)
ED: AG
DATE: Friday, May 12, 2017

MULEBA

Baadhi ya wazee wa kitongoji cha Nyamiranda B kata ya Kyebitembe wilayani Muleba mkoani Kagera bado wanaendelea kutaabika katika kupata huduma za matibabu kutokana na ukosefu wa vitambulisho vya kutibiwa bure

Wakiongea na redio kwizera wazee hao ambao ni Bw Terentin Michael, Bi Juster Adrian na Bw William Rushaye wamesema kuwa wanapata adha kubwa hivyo wameiomba serikali kuwapatia vitambulisho vya kutibiwa bure 

Wamesema kuwa adha wanayoipata ni pamoja na kulipia matibabu pamoja na wahudumu kutowajali pale wanapokuwa kwenye vituo vya afya

Insert….Wwazee
Cue…..in
Cue…..out

Kwa upande wake Afsa miradi wa shirika la wazee wilayani Muleba Bw Jovinary Frances amesema mikakati ambayo wamekwishafanya kwa sasa ni kuhakikisha wazee hao wanaenda kwa mwenyekiti wa kitongoji ama mtendaji ili wapatiwe barua ya kuwatambulisha kutibiwa bure.


SOURCE: Taarifa, AG (Kanusho)
ED: AG
DATE: Friday, May 12, 2017

DODOMA

Ofisi ya Rais -Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya umri wa mtu kuajiriwa serikalini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini ofisi ya Rais -Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, habari hizo si za kweli na ni za kupuuzwa.

Taarifa hizo zilikuwa zikisema kuwa “Waziri wa Utumishi Angella Kairuki amesema kama wewe umemaliza chuo kikuu lakini umri wako umevuka miaka 30 endelea kusubiri ajira, sasa hivi tunachukua walio na umri wa miaka 30 kwani idadi yao ni kubwa zaidi”

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais -Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi Angella Kairuki amedai kuwa hajasema maneno hayo hivyo wananchi na wadau wengine wanapaswa kupuuza habari hiyo.

Mwisho. Sikiliza taarifa ya Habari kila siku Saa sita kamili mchana,Saa mbili kamili usiku na Saa tano kamili usiku taarifa ya habari ya saa 24 zilizopita-Ngara 97.9 FM,Kibondo 93.6 FM,Kasulu,Buhigwe,Uvinza,Kigoma Mjini,DRC na Burundi 94.2 FM,Kahama 97.3 FM,Geita 90.5 FM na Bukoba 97.7 FM - Pia mtandao wa Internet na Apps ya Tune In/Radio Kwizera.


Wasiliana/News Desk, Ngara Kagera.
Chief News Editor
Ms AuleriaGabriel
auleria@radiokwizera.com
Mobile: +255 769722554

Post a Comment

0 Comments