habari Mpya


Rekodi ya Manchester United baada ya Ubingwa wa Kombe la Europa 2016/2017.

Picha ya Furaha ya Ubingwa 2016/2017.

Manchester United wameshinda fainali ya Kombe la Europa kwa kuifunga Ajax Amsterdam kwa mabao 2-0 mjini Stockholm Sweden.

Magoli ya Mchezaji Paul Pogba na Hendrick Mkhitaryan yameipa Man United sio tu Kombe bali pia nafasi ya kucheza Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao wa 2017/2018.

Manchester United sasa wanaungana na Chelsea, Tottenahm na Manchester City katika kucheza Klabu Bingwa Ulaya.

Pia ushindi huu utawaingizia kitita cha takriban Pauni milioni 50.


Hili ni kombe la Pili kwa Kocha Mourinho anashinda na Man United katika msimu wake wa kwanza. Man United walishinda Kombe la Ligi mwezi Februari.

Pia -Jose Mourinho ameshinda Fainali zote 4 za Ulaya alizotinga kama Meneja akitwaa UEFA CUP 2003 na UEFA Champions League 2004 akiwa na FC Porto, na UEFA Champions League 2010 akiwa na Inter Milan.

Mourinho amedumisha rekodi yake ya 100% ya ushindi dhidi ya Ajax katika Mechi zote 7 alizocheza nao.

Kocha Jose Mourinho.

Man United wamejumuika na Ajax, Bayern Munich, Chelsea na Juventus kuwa Klabu pekee zilizonyakua Makombe yote ya UEFA huko Ulaya.

-Vikombe hivyo ni UEFA Champions League, UEFA Cup Winners' Cup, UEFA Cup/UEFA EUROPA League.

Jose Mourinho Ameeleza: “Ni mwisho wa Msimu mgumu. Lakini ni Msimu mzuri mno!”

Mourinho alieleza: “Sasa tuna heshima ya kucheza UEFA SUPER CUP na Bingwa Mpya wa UEFA Champions League kati ya Real Madrid au Juventus watakaocheza fainali ya Champions League June 03,2017, kwa hiyo Msimu huu ulikuwa mzuri mno!”

Post a Comment

0 Comments