habari


Rasmi sasa Serengeti Boys anahitaji sare kwenda World Cup 2017-India.

Wachezaji wa Tanzania wakishangilia bao la kwanza leo Uwanja wa L'Amittee mjini Libreville.

Timu ya Serengeti Boys huenda ingepata ushindi wa magoli zaidi ya mawili kama ingetumia vizuri nafasi zilizotengenezwa wakati ikipambana na Angola kwenye mechi ya pili ya Kundi B ya michuano ya AFCON U17.

Kocha msaidizi wa Serengeti Boys Oscar Mirambo amesema, wachezaji wanapaswa kufahamu umuhimu wa nafasi zinazopatikana na kuzitumia.

Serengeti Boys ilishinda magoli 2-1 dhidi ya Angola na kufikisha pointi 4 sawa na Mali ambao nao walishinda bao 2-1 dhidi ya Niger.
 
Tanzania walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake tegemeo Yohana Oscar Mkomola dakika ya tano kwa kichwa baada ya krosi ya Enrick Vitalis Nkosi kabla ya Francisco Chilumbo kuisawazishia Angola dakika ya 19.

Abdul Suleiman aliwapa raha Watanzania kwa kufunga bao zuri la ushindi dakika ya 69 akimalizia pasi ya Yohanna Oscar Nkomola.
Mchezo huo wa pili wa Kundi B kati ya Mali dhidi ya Niger umemalizika kwa Mabingwa watetezi Mali kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ambayo yamefungwa na nahodha wao Mohamed Camara na Hadji Drame wakati Niger wameambulia goli moja lililofungwa na Habibou Sofiane.

Ushindi huo wa Mali unawafanya kuwa sawa kwa point na Tanzania na kuwa sawa kwa kila kitu kwa maana ya magoli ya kufunga na kufungwa, Tanzania wana point nne wakifunga magoli mawili na kuruhusu moja sawa na Mali wakati Mali na Angola na wenye wakisalia na point moja wakifanana pia kwa kila kitu, Tanzania sasa inahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo wa mwisho dhidi ya Niger.

Jumapili May 21, 2017, zitachezwa mechi za mwisho za makundi na timu nne (mbili kutoka kila kundi) zitasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.

Post a Comment