habari Mpya


Benki ya CRDB tawi la Ngara mkoani Kagera Yaipiga Jeki Sekondari ya Mt. Alfred Rulenge Sh1.2 milioni ili Kukuza Mtaji wa Ujasiriamali.

Meneja wa benki ya CRDB tawi la Ngara mkoani Kagera akipata maelezo ya utengenezaji wa vitambaa vya batiki kutoka kwa LITHA MPANJU,  Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mtakatifu Alfred Rulenge inayomilikiwa na jimbo katoliki la Rulenge Ngara mkoani humo   kwenye mahafali ya 14 ya kidato cha Sita yaliyofanyika shuleni hapo  May 13 , 2017 kupitia elimu ya ujasiliamali  ambapo amechangia wanafunzi wa shule hiyo Sh1.2 milioni kuongeza mtaji wa kupata vitendea kazi katika ujasiliamali.Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtakatifu Alfed Rulenge hujishughulisha na elimu ya ujasiliamali ambapo hutengeneza sabuni za maji na miche wakiongozwa na mwalimu wao wa ujasiliamali Godbert Kalezibwaki , kwa ajili ya usafi wa mavazi na kusafisha miundombinu mbalimbali kama vyoo, ambapo kwa sasa wanahitaji usajili baada ya kukaguliwa na TBS

Picha/ HABARI na Shaaban Ndyamukama.

Katika hatua nyingine Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Ngara mkoani Kagera Ernest Chacha amewahimiza wahitimu kufanya kazi  halali zenye kuwaongezea mapato kiuchumi ambapo amefurahia uanzishwaji wa elimu ya ujasiliamali  shuleni hapo

Akihutubia wanafunzi na wahitimu pamoja na wazazi au walezi waliohudhuria mahafali hayo Meneja huyo  ameendesha harambee ya kupunguza changamoto za  miundombinu na kupatikana kiasi cha Sh1.2 milioni naye kuchangia kiasi kama hicho akiahidi kuingiza fedha hizo kwenye akauti ya shule itakayofunguliwa kupitia benki ya CRDB.

Jumla ya  wanafunzi 25 wa kidato cha sita wamehitimu kidato hicho shuleni hapo kati yao ni wasichana tisa na wavulana 16 baada ya kuanza mwaka 2015  wkiwa wanafunzi 32 kati yao wavulana 21 na wasichana 11 lakini baadhi yao hawakuweza kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali za kimazingira.

Post a Comment

0 Comments