habari


Vyeti feki 9,932 Tanzania,Nafasi zao Kutangazwa Ajira Mpya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki wakiminya kitufe kuashiria maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM hapo Jana April 28,2017 katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia viongozi mbalimbali, wanafunzi wa UDOM, pamoja na watumishi wa Umma mara baada ya kupokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti  kwa watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Jana Aprili 28, 2017 amewafuta kazi wafanyikazi 9,932 wa serikali kwa kuwa na vyeti bandia vya elimu.

Amewaagiza kuacha kazi ifikiapo Mei 15,2017 la sivyo wakamatwe na kushtakiwa.

Hatua hiyo inajiri baada ya wafanyikazi hao kupatikana na vyeti bandia vya shule.

Kulingana na ripoti iliyopokelewa na rais Magufuli, inaonyesha wafanyikazi 9,932 wa serikali walipatikana na vyeti bandia vya shule.

Akikabidhi taarifa hiyo kwa Rais Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Rais amesema kuwa, Wizara yake iliagiza NECTA kuhakiki vyeti vya kidato cha nne, cha sita na vya uwalimu.

“Jumla ya watumishi wa umma 435,000 wamefanyiwa uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma, Watumishi 9932 kati ya watumishi waliohakikiwa walikutwa na vyeti vya kughushi, Vyeti vyenye utata. Vyeti 1538 vilikuwa vikitumiwa na jumla ya watu 3076”

Akizungumza baada ya kupata ripoti hiyo, rais Magufuli amewapatia maafisa walio na vyeti hivyo wiki chache za kujiuzulu la sivyo washitakiwe.

Rais Dk. Magufuli pia ameziagiza mamlaka husika kujumuisha nafasi 9,932 za ajira ambazo zimeachwa wazi na watumishi wa umma walioghushi vyeti, kwenye ajira mpya zaidi ya elfu 52 za serikali ili ziweze kuchukuliwa na watu wenye sifa na uwezo wa kumudu nyadhifa zilizoachwa.
 
Pia ameyataka magazeti nchini humo kuchapisha majina ya maafisa hao.

Post a Comment