habari


Robert Huth Ajifunga na kuipa Arsenal bao 1-0 dhidi ya Leicester City -EPL 2016/2017.uth

Jana April 26,2017 katika Uwanja wa Emirates Jijini London, Arsenal walifanikiwa kuwafunga Mabingwa watetezi wa Ligi kuu England, Leicester City bao 1-0 , Bao la dakika ya 86 la mchezaji Robert Huth aliejifunga mwenyewe.

 Huko Selhurst Park Jijini London, Crystal Palace walilala 1-0 kwa Tottenham Hotspur ambao sasa wamejizatiti Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Chelsea walioshinda bao 4-2 dhidi ya Southampton.

Bao la ushindi la Mechi hiyo lilifungwa Dakika ya 78 na Christian Eriksen.


Nako huko Riverside Wenyeji Middlesbrough waliitungua Sunderland 1-0 kwa Bao la Dakika ya 9 la Marten De Roon.

Leo April 27, 2017  ipo Mechi ya EPL na kazi hiyo kubwa ipo huko Etihad ambako iko Dabi ya Jiji la Manchester kati ya Man City na Man United Timu ambazo zinapishana Pointi 1 tu wakati Man City wapo Nafasi ya 4 na Man United Nafasi ya 5.

Alhamisi Aprili 27,2017.

2200 Manchester City v Manchester United    


Post a Comment