habari Mpya


Picha-Risasi 193 za silaha Zaokotwa na Jeshi la Polisi Ngara katika daraja la mto Ruvubu.

Risasi zikionekana kutupwa.

Jumla ya Risasi 143 za silaha aina ya Raifo, risasi za Pisto 13, Risasi za shotgun 33 pamoja na maganda manne ya risasi za Shortgun jana,April 19,2017, zimeokotwa katika daraja la mto Ruvubu kitongoji cha Mkanyagari kijiji cha Kasharazi wilayani Ngara mkoani Kagera.

Akizungumza na Radio Kwizera, Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Ngara,Mkoani Kagera Bw Abeid Maige amesema risasi hizo zimeokotwa majira ya saa kumi jioni na taarifa za kuwepo kwa risasi hizo imetolewa na kijana Gerald James mkazi wa kitongoji hicho na haijajulikana watu waliozidondosha.

Amesema risasi hizo zimetupwa usiku wa kuamkia jana ambapo watu hao walikuwa na lengo la kuzitupa ndani ya mto ili kupoteza ushahidi.

Pia Bw Maige amesema wamehakikisha hakuna mabaki ya risasi katika eneo hilo na amewataka wakazi wa Ngara hasa wa vijijini kuwa makini na kutoa taarifa kwa viongozi wao pale wanapobaini uwepo wa vitu vinavyoashiria kuhatarisha maisha yao
Juu na chini piachani  ni Wananchi wa kijiji cha Kasharazi wilaya ya Ngara mkoani Kagera wakichunguza Risasi 193 zilizookotwa   jana April 19, 2017 baada ya kutelekezwa  na watu wasiojulikana kando ya daraja la mto Ruvubu barabara kuu ya Ngara hadi eneo la K9 katika kijiji hicho.
Askari polisi wa wilaya ya Ngara makao makuu ya polisi ya wuilaya mkoani Kagera wakishuhudia  Risasi 193 za silaha mbalimbali zinazotumika kuuwa wanyama kwenye hifadhi baada ya kuokotwa kandokando ya mto Ruvubu katika daraja kuu la Kasharazi kutoka mjini Ngara kuelekea Benaco wilayani Ngara April 19, 2017 saa 10 alasiri.

Kandokando ni Mto Ruvubu katika daraja kuu la Kasharazi kutoka mjini Ngara kuelekea Benaco wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Post a Comment

0 Comments