habari Mpya


La Liga 2016/2017-FC Barcelona na Real Madrid wakabana koo wote wakiwa na Pointi sawa 78 baada ya kushinda Mechi kwa kishindo kikuu.

Mchezaji James Rodriguez na wenzake wakifurahia baada ya kuifungia timu yake ya Real Madrid mabao mawili dakika za 14 na 66 katika ushindi wa Real Madrid wa  bao 6-2 dhidi ya wenyeji Deportivo La Coruna usiku wa jana April 26, 2017 kwenye mchezo wa La Liga Uwanja wa Manispaa ya Riazor.


Mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa na Alvaro Morata dakika ya kwanza, Lucas Vazquez dakika ya 44, Isco dakika ya 77 na Casemiro dakika ya 87 wakati ya wenyeji yalifungwa na Florin Andone dakika ya 35 na Joselu dakika ya 84. 

Kocha Zinadine Zidane hakutumia wachezaji tisa aliowaanzisha Jumapili wakifungwa 3-2 na FC Barcelona, akiwemo Cristiano Ronaldo.
Kwa matokeo hayo  Ligi Kuu ya Spain, inaingia patamu sana kwa Mechi kubakia chache na Mabingwa Watetezi FC Barcelona na Real Madrid, kukabana koo wote wakiwa na Pointi sawa 78 baada ya kushinda Mechi zao kwa kishindo kikuu.

FC Barcelona wamebakisha Mechi 4 na Real Madrid Mechi 5.

Barcelona, ambao ndio wanaongoza Ligi kwa Ubora wa Magoli, Jana waliitandika Timu ya Mkiani Osasuna 7-1 huko Nou Camp huku Lionel Messi akifunga Bao 2 na nyingine kupachikwa na Andre Gomes, Bao 2, Parco Alcacer, 2 na Penati ya Javier Mascherano.

Bao pekee la Osasuna lilifungwa na Roberto Torres.

Post a Comment

0 Comments